Nchi za Afrika zenye amani zaidi kwa mwaka 2024

0
29

Amani ni hali ya utulivu, usalama, na uhakika wa maisha bila vitisho vya ghasia au migogoro. Ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu, ustawi wa jamii, na ukuaji wa uchumi.

Amani sio tu kutokuwepo kwa vita au ghasia, bali pia ni hali ya usawa na haki katika jamii. Inajumuisha hali ya kuridhika, mshikamano wa kijamii, na utulivu wa kiroho. Amani inamaanisha kuwepo kwa mazingira ambapo watu wanaweza kuishi kwa uhuru, kuheshimiana na kushirikiana kwa ajili ya manufaa ya wote.

Ripoti mpya ya Global Peace Index ya mwaka 2024, imebainisha kwamba kwa sasa dunia iko njia panda, na bila juhudi za pamoja kuna hatari ya kuongezeka kwa migogoro mikubwa.

Nchi 10 za Afrika zinazokabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, kiusalama na kisiasa kwa sasa

Katika miezi minne ya kwanza ya mwaka 2024, vifo vinavyotokana na migogoro duniani vilifikia 47,000, na ikiwa kiwango hicho kitaendelea zaidi, itakuwa ni idadi kubwa zaidi ya vifo vitokanavyo na vita tangu mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994.

Zifuatazo ni nchi 10 za Afrika zenye amani zaidi mwaka 2024;

  1. Mauritius
  2. Madagascar
  3. Botswana
  4. Ghana
  5. Zambia
  6. Namibia
  7. Tanzania
  8. Sierra Leone
  9. Liberia
  10. Angola
Send this to a friend