Nchi za Afrika zenye kiwango kikubwa zaidi cha madeni

0
53

Afrika kuna jumla ya nchi 54, ambapo 34 kati ya hizo zipo katika orodha ya nchi zinazodaiwa zaidi, Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zimeeleza.

Katika orodha hiyo inayojumuisha nchi 40 duniani kote, nchi za Afrika zilizoorodheshwa zina idadi ya watu wapatao milioni 760.

Nchi hizo ni Ghana, Ethiopia, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Comoros Islands, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Congo.

Nyingine ni Ivory Coast, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Tanzania, Togo, Uganda na Zambia.

Taasisi hizo za kifedha duniani mwaka 1996 zilizindua mpango wa kuzinusuru nchi zenye madeni makubwa kuhakikisha kuwa hakuna nchi masikini duniani ambayo itakabiliwa na mzigo mkubwa wa deni ambalo haiweza kuumudu.

WB na IMF pamoja na taasisi nyingine za kifedha hufanya kazi kwa kushirikiana na serikali za nchi husika kupunguza madeni ya nje kufikia katika kiwango himilivu.

Ili nchi iweze kuwekwa katika mpango huo lazima ikidhi vigezo mbalimbali ikiwemo kuwa na uwezo wa kukopa kutoka wakala wa kimataifa wa maendeleo wa Benki ya Dunia na iwe nchi yenye mzigo wa deni ambao hauwezi kutatuliwa kupitia njia za kawaida.

Aidha, nchi lazima ioneshe rekodi yake ya mkakati wa kimaendeleo na sera za kuchochea maendeleo pamoja na kuwa na mpango mkakati wa kupunguza umasikini.

Send this to a friend