Nchi za Afrika zinazoongoza kwa wanandoa kupeana talaka

0
46

Talaka ni mchakato rasmi wa kuvunja ndoa kisheria. Ni uamuzi mgumu ambao unaweza kuathiri maisha ya wanandoa wote wawili, watoto wao (ikiwa wapo), familia zao, na jamii kwa ujumla.

Ingawa ni jambo la kusikitisha, talaka inaweza kuwa ni hatua muhimu kwa wanandoa wanaokabiliwa na matatizo yasiyoweza kutatuliwa ndani ya ndoa yao.

Bara la Afrika mara nyingi linasifiwa kwa wanandoa kudumu katika uhusiano thabiti wa kifamilia, lakini kwa sasa linapitia mabadiliko katika mazingira yake ya ndoa ikichangiwa na utandawazi pamoja na usasa.

Mambo 6 ya kufanya kumrudisha mwanamke aliyekukataa

Ingawa data kuhusu talaka barani Afrika ni ndogo, ripoti ya Wisevoter inatoa takwimu za talaka barani humo.

Hizi Nchi za Kiafrika zenye kiwango cha juu zaidi cha talaka (kwa kila watu 1000);

  1. Libya: 2.5
  2. Misri: 2.2
  3. Mauritius: 1.7
  4. Algeria: 1.6
  5. Seychelles: 1.5
  6. Sudan: 1.5
  7. Afrika Kusini: 0.6
Send this to a friend