Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 ilimalizika Jumapili, huku nchi kadhaa zikitwaa medali kuanzia dhahabu hadi shaba, na nchi nyingine nyingi zikiondoka mikono mitupu.
Marekani ndiyo iliyoongoza kutwaa medali nyingi, kwa kujinyakulia medali 40 za dhahabu na jumla ya medali 126, ikiishinda China iliyopata medali 91, zikiwemo medali 24 za shaba.
Mwaka huu, ni mataifa 12 pekee ya Kiafrika yaliyofanikiwa kuingia kwenye jedwali la medali ambapo Kenya imeongoza kwa jumla ya medali 11: 4 za dhahabu, 2 za fedha na 5 za shaba na kufuatiwa na Afrika Kusini.
Zifuatazo ni nchi za Kiafrika zilizo na medali nyingi zaidi katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024:
S/N | NCHI | DHAHABU | FEDHA | SHABA | JUMLA |
1 | Kenya | 4 | 2 | 5 | 11 |
2 | Afrika Kusini | 1 | 3 | 2 | 6 |
3 | Ethiopia | 1 | 3 | 0 | 4 |
4 | Algeria | 2 | 0 | 1 | 3 |
5 | Misri | 1 | 1 | 1 | 3 |
6 | Tunisia | 1 | 1 | 1 | 3 |
7 | Botswana | 1 | 1 | 0 | 2 |
8 | Uganda | 1 | 1 | 0 | 2 |
9 | Morocco | 1 | 0 | 1 | 2 |
10 | Côte d’Ivoire | 0 | 0 | 1 | 1 |
11 | Cabo Verde | 0 | 0 | 1 | 1 |
12 | Zambia | 0 | 0 | 1 | 1 |