Ndanda FC yaingizwa sokoni

0
64

Ndanda Fc maarufu ya mkoani Mtwara ambayo inashiriki ligi kuu daraja la kwanza inauzwa rasmi kutokana na kukosa fedha za kujiendesha.

Mkurugenzi wa Bodi ya timu hiyo, Said Limbega amesema uongozi umeridhia kuiuza kwa kuwa imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo uwezo wa kifedha, kwani timu hiyo inapitia kipindi kigumu katika kushiriki kwenye mashindano.

Amesema timu, maarufu Wanakuchele inauzwa bila masharti na mwekezaji au mtu yeyote anayeitaka afike kuinunua na atakuwa na hiari ya kuiacha timu hiyo Mtwara au kuipeleka mkoa wowote.

Send this to a friend