Ndege iliyoshikiliwa Afrika Kusini ina vifaa vya ulinzi wa Rais- Wakili Nkhwashu

0
17

Tanzania imeitaka Mahakama Kuu ya Gauteng ya Nchini Afrika Kusini kufanya jitihada za haraka katika kujibu mapingamizi yao ya kutaka kuachiwa kwa ndege ya ATCL inayoshikiliwa Afrika Kusini

Wakili Victor Nkhwashu, Mwanasheria wa Serikali aliyechaguliwa kusimamia suala hilo amesema wamewasilisha viapo vya vya kuomba utolewaji wa uamuzi wa mapema kwani ndege iliyoshikiliwa inatumiwa na Rais wa Tanzania

Aidha, Wakili huyo amedai kuwa siku za hivi karibuni, Rais ameshindwa kutimiza majukumu yake ya Kimataifa kutokana na ndege hiyo kuzuiwa katika uwanja wa ndege wa Kimaifa wa OR Tambo

Amesema kwa kuwa ndege hiyo hutumika kwa safari za kiofisi za Rais, ina vifaa nyeti vya ulinzi ambavyo hutumiwa na Rais akisafiri, hivyo kuiacha ndege hiyo ugenini kwa muda mrefu kunaweza kusababisha taarifa muhimu kuingiliwa, na ni hatari kwa mhimili wa serikali (executive) wa dola.

Aliongeza kuwa, kwa muda ndege hiyo inavyoshikiliwa inaisababishia Kampuni ya ATCL na Watanzania kwa ujumla upotevu mkubwa wa mapato kutokana na kuahirishwa kwa safari za abiria na zile za Rais.

HT: Daily News

Send this to a friend