Ndege tatu za ATCL zasimamishwa kuendelea na kazi

0
64

Serikali imesema kusimamishwa kwa safari za ndege tatu za Airbus 220 za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) zimetokana na hitilafu za kiufundi, hivyo kutokana na hali hiyo kampuni iliyozitengeneza zimeagiza zisimamishwe hadi pale hitilafu hiyo itakaporekebishwa.

Akifafanua suala hilo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema hitilafu hiyo si ya ndege za ATCL pekee, bali na za kampuni nyingine zilizonunua ndege za aina hiyo.

Ameongeza kuwa ni utaratibu wa kawaida kwamba mtengenezaji wa ndege anapogundua hitilafu kwenye ndege anatoa taarifa ya kusitisha matumizi ili kutatua changamoto iliyojitokeza, na kwamba utaratibu huo si kwa Tanzania pekee bali ni kwa nchi zote duniani.

Nauli mpya za Mwendokasi zitakazoanza kutumika kuanzia Januari 16, 2023

Hata hivyo, Msigwa amesema Serikali inaendelea kuwasiliana na kampuni husika iliyotengeneza ndege hizo ili wazitengeneze na kumaliza hitilafu hiyo ili kuendelea kutoa  huduma.

Send this to a friend