Ndege ya Maafisa Usalama wa Rais Ramaphosa yanyimwa kibali kuelekea Urusi

0
41

Takribani maafisa wa usalama 120 kutoka Huduma ya Ulinzi ya Rais (PPS), kikosi kazi cha SAPS na vitengo vingine maalumu watarejea Afrika Kusini siku ya Jumapili baada ya ndege iliyokodishwa na serikali ya Afrika Kusini kushindwa kupata kibali cha kuruka kuelekea Urusi.

Rais Cyril Ramaphosa na viongozi wengine wa Afrika wanategemea kukutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin huko St. Petersburg nchini Urusi Jumamosi mchana baada ya kukutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky mjini Kyiv siku ya Ijumaa.

Watu 25 wauawa shuleni nchini Uganda

Wana usalama walipaswa kutumwa Kyiv na St Petersburg kabla ya kuwasili kwa Ramaphosa ili kuhakikisha usalama wake, lakini kikosi kizima ikiwa ni pamoja na mkuu wa PPS, Jenerali Wally Rhoode walikwama katika Uwanja wa Ndege wa Chopin wa Warsaw, Poland kwa zaidi ya saa 26 wakati Rais akiwa nchini Ukraine.

Mamlaka ya Poland imesema imekataa Waafrika Kusini kuingia Poland kwa sababu ya kutokamilika kwa kibali, pamoja na kuhusishwa kwa shehena ya silaha ambazo ndege ilikuwa imebeba.

Kibali cha ndege kuondoka Warsaw kwenda St Petersburg pia kilikataliwa, ikimaanisha kuwa SAA Airbus (A340-300) ambayo iliondoka kwenye Kambi ya Jeshi Jumatano usiku ikiwa na wana usalama 120 na wafanyakazi wa shirika la ndege, itarejea Pretoria bila kutimiza lengo.

Send this to a friend