Ndege ya Tanzania iliyokuwa imeshikiliwa Uholanzi yaachiwa 

0
62

Ndege aina ya Airbus A220 ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishiliwa nchini Uholanzi imeachiwa na kurejea nchini.

Hayo yameelezwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

“Leo niko hapa kuwapa habari njema, siku chache zilizopita niliwajulisha kuna ndege yetu tulikuwa na kesi nchini Uholanzi ikakamatwa, ilikuwa chini ya mikono ya sheria bahati nzuri tumefanya mazungumzo na jambo limekwenda vizuri, ndege yetu imerudi jana jioni iko Tanzania,” amesema.

Ameongeza kuwa “chuma kimerejea kikoa Tanzania, tunaendelea kuimarisha shirika letu, mambo yetu yatakuwa yanaendelea kuwa mazuri.”

Send this to a friend