Ndege yachelewa kuondoka baada ya abiria kutupa sarafu kwenye injini

0
51

Ndege ya shirika la ndege la China Southern Airlines imelazimika kuchelewa kwa zaidi ya saa nne baada ya abiria mmoja (jina halikuwekwa wazi) kutupa sarafu kwenye injini.

Awali, ndege hiyo ilipangwa kuondoka kutoka mji wa kusini wa Sanya nchini China kwenda Beijing saa 4 asubuhi lakini iliondoka saa nane mchana.

Katika video iliyosambaa kwenye vyombo vingi vya habari, mhudumu wa ndege ameonekana akimhoji abiria anayeaminika kurusha sarafu hizo, akimuuliza ni sarafu ngapi zilitupwa kwenye injini na abiria huyo alisikika akisema “sarafu tatu hadi tano.”

ATCL yafafanua hitilafu iliyotokea kwenye injini ndege ikiwa angani

Shirika hilo la ndege limesema baada ya kufanya ukaguzi wa kiusalama, walifanikiwa kuzipata sarafu hizo japokuwa halikufafanua idadi kamili ya sarafu zilizopatikana, huku mtuhumiwa akichukuliwa na pollisi.

Aidha, katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii shirika hilo la ndege limelaani na kutoa onyo dhidi ya kitendo hicho kwa kueleza kuwa, kufanya hivyo kunaweza kusababisha athari mbaya katika usalama wa anga.

Send this to a friend