Ndege ya Delta Airlines kutoka Atlanta kwenda Barcelona imelazimika kugeuka baada ya abiria mmoja kupata ugonjwa wa kuharisha na kusababisha harufu mbaya iliyotanda ndani ya ndege.
Ndege hiyo DL194 ilikuwa tayari imeondoka Georgia siku ya Ijumaa saa 2:47 usiku, kulingana na sauti zilizorekodiwa kati ya rubani na mamlaka ya udhibiti wa anga, rubani aliomba kugeuka saa mbili tu baada ya kuruka katika safari ya saa nane kuelekea Uhispania.
Kwenye rekodi, rubani aliiambia mamlaka ya udhibiti wa anga, “hili ni suala la hatari ya kibiolojia. Tumekuwa na abiria ambaye amekuwa na ugonjwa wa kuhara kwenye ndege, kwa hivyo wanataka turudi Atlanta,” alisema rubani.
Kwa bahati nzuri, ndege hiyo ilisafishwa vizuri na iliweza kukamilisha safari yake siku iliyofuata.