Ndege ya United Airlines aina ya Boeing 787 iliyokuwa ikisafiri kutoka Los Angeles hadi Shanghai ililazimika kurejea nyuma takriban saa mbili baada ya kuanza safari, baada ya kugundulika kuwa mmoja wa marubani hakuwa na pasi ya kusafiria.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa shirika hilo, ndege hiyo ilielekezwa San Francisco, ambapo abiria walipatiwa fidia na vocha za chakula, kisha rubani mwingine alikabidhiwa nafasi ya kuendeleza safari. Hatimaye, ndege hiyo iliwasili Shanghai ikiwa imechelewa kwa takriban saa sita nyuma ya ratiba.
DRC yaondoa Visa kwa Tanzania
Yang Shuhan, abiria wa Kichina aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo, aliiambia CNN kuwa alisikia sauti ya rubani ikionyesha mfadhaiko mkubwa kupitia kipaza sauti, akisema kuwa amesahau pasipoti yake.
Mabadiliko hayo hayakuishia kwenye ndege hiyo pekee, bali pia abiria waliokuwa kwenye ndege ya kurudi ya United Airlines 199 kutoka Shanghai kwenda Los Angeles walikumbwa na matatizo kutokana na kuchelewa kwa ndege iliyoingia.