
Watu 15 wamejeruhiwa nchini Korea Kusini baada ya mabomu yaliyodondoshwa na ndege za kivita kuanguka katika eneo la raia na kusababisha uharibifu wa nyumba na kanisa wakati wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi mjini Pocheon.
Jeshi hilo limesema litaanzisha kamati maalum kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kutathmini kiwango cha uharibifu uliosababishwa kwa raia.
Pia, imeeleza kuwa ndege hizo zilikuwa zinashiriki katika mazoezi ya pamoja ya risasi za moto halisi kati ya jeshi la anga na jeshi la nchi kavu.
Aidha, afisa mmoja wa Wizara ya Ulinzi, ambaye pia hakutajwa jina, amewaambia waandishi wa habari kwamba uchunguzi zaidi unahitajika ili kubaini sababu iliyomfanya rubani wa ndege ya pili ya KF-16 pia kudondosha mabomu katika eneo la raia.