Ndejembi awataka wanafunzi vyuo vikuu kutowatega kingono wahadhiri

0
58

Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deogratius Ndejembi amewataka wanafunzi kutowatega wahadhiri wao kingono ili kuwaepusha kuingia katika vitendo viovu ikiwemo rushwa ya ngono.

Akizungumza hapo jana wakati akifungua kongamano la kukuza maadili na mapambano dhidi ya rushwa lililoshirikisha Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) amebainisha kuwa rushwa ya ngono ni miongoni mwa changamoto zinazovikumba vyuo mbalimbali duniani.

“Madhara ya rushwa ya ngono ni wanafunzi wasiostahili wanaweza kupewa alama nyingi kuliko wanazostahili, hii inaweza kumhusu mwalimu wa kiume akishirikiana na wanafunzi wa kike,” amesema Ndejembi.

Aina ya kozi za kusoma zitakazokuwezesha kupata ajira kwa urahisi

Ameeleza kuwa “wahadhiri wa kike wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kiume na kwamba hasara ni kuzaliwa kwa wasomi ambao hawana tija na kuwanyima haki wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao.”

Aidha, amewataka wanafunzi kuendelea kutoa taarifa za wanaojihusisha na vitendo hivyo bila kuwasingizia, ili hatua stahiki zichukuliwe kwakuwa Serikali inataka kutokomeza vitendo hivyo katika taasisi za elimu ya juu.

Send this to a friend