Ndoa 1 huvunjika kila siku wilayani Temeke

0
50

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema anashangazwa kuona ndoa nyingi zinavunjika katika jamii ndani ya muda mfupi.

Waziri amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema katika kipindi cha miezi tisa, ndoa takribani 350 zimevunjika katika Wilaya ya Temeke pekee.

Wanaume washauriwa kusimamia wake zao wanyonyeshe

Ameongeza kuwa hali hiyo si nzuri, kwani takwimu hizo ni kwa manispaa moja na hajajua hali ya nchi nzima ikoje, na kwamba viongozi wa dini wana kazi ya kufanya kutokana na mmomonyoko wa maadili unaochangia ndoa nyingi kuvunjika.

“Ndoa hizo zinafungwa na sherehe kubwa na kujipamba, na viongozi wa dini wakiwa wanaziongoza kwa baraka lakini hazichukui muda zinavunjika. Naomba sasa viongozi wangu mkaangalie hili katika kufundisha, kwani ndoa kuvunjika ni chukizo la Mungu,” amesisitiza Simbachawene.

Send this to a friend