Ndoa miaka 14: BAKWATA yaelezea kwa kina   

0
13

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema Serikali kuzuia mtoto wa umri wa miaka 14 kuolewa ni kuzuia kumuabudu Mungu na kumruhusu shetani aingie kati.

Akizungumza na Swahili Times, Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikhe Hassan Chizenga amepinga kubadilishwa kwa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, hasa kipengele kinachoruhusu binti wa miaka 14 kuolewa kwa idhini ya mahakama katika mazingira maalum.

“Ndoa ina maana mtoto wa kike na wa kiume waruhusiwe kufanya tendo la ndoa, wawe wapenzi. Ikifanywa akatajwa Mungu na usimamizi wa wazazi kosa, lakini ikifanywa kiholela bila usimamizi wa wazazi ni sawa, mimi naona hiki ni.. [akitaja neno kali].

Kama Serikali inagawa kondumu ili kuwakinga na maambukizi, hivyo basi imekubali ndoa ya shetani iwepo lakini ya Mungu isiwepo. Sera ya nchi yetu inakubaliana kwamba haja ya kufanya hivyo [kujamiiana] ipo,” amesema.

Tahadhari yatolewa kwa wanawake wanaoweka tumbaku sehemu za siri

Aidha, amesema dini haijataka kila mtoto aozeshwe akiwa na umri wa miaka 14, ila pale dharura itakapolazimu basi asizuiwe na kulazimishwa kuzini kwa sababu sheria inamlazimu.

“Sisi tunahamasisha watoto wasome. Wale ambao wako katika uwezo wa kuweza kusoma na wazazi wanawaendeleza wasome, ile elimu yenyewe automatically [moja kwa moja] itamfanya mtu asiwe na kiu ya lile jambo. Lakini kuna huyu mtoto ambaye masikini darasani haelewi akifundishwa hafahamu, ana miaka kumi na, na pengine kapewa umbo zuri lapendeza. [..] Sheria ya ndoa 1971 haijamzuru yeyote,” ameeleza.

Hata hivyo Chizenga ameongeza kuwa ndoa zinazofungwa hufanyika chini ya usimamizi wa wazazi hivyo wanaweza kuwaangalia na kuwaelekeza majukumu mbalimbali.

Send this to a friend