Ndoa yavunjia kisa mke kuhongwa bia moja na hawara

0
12

Wakati jamii ikikemea ukatili ndani ya ndoa, bia moja imesabibisha ndoa kuvunjika huko wilayani Urambo mkoa wa Tabora na mke kubaki na majeraha makubwa ya kuumizwa kwa kipigo na mume wake.

Akisimulia tukio hilo, Bernadeta Robert aliyedai kuachika amedai mumewe alimtuhumu kuhongwa bia na hawara, ndipo akamshambulia kwa ngumi na mateke kisha kumfukuza nyumbani kwake na kumlazimu kuishi kwa jirani.

“Alinipiga kiasi cha kupata maumivu makali, kisha akaniamuru niondoke na yeye ataoa mke mwingine mzuri zaidi yangu,” amedai.

Amesimulia kwamba mumewe alimpa kipigo hicho mwezi mmoja tangu ajifungue hivyo kusababisha kutokwa na damu sehemu za siri, kuumiza jicho, shingo na kukohoa damu.

Amesema alirudi kijijini kwa wazazi wake akapewa barua ya kwenda kutibiwa kisha kurejea kwa mume wake, lakini cha ajabu alikmkuta akiwa mke mwingine katika nyumba waliyoijenga pamoja huku akimkana kuwa si mkewe na kumuamuru aondoke.

Amedai baada ya kushindwa kusuluhisha Ustawi wa Jamii na Baraza la Kata, aliamua kufungua kesi ya madai ya mali mahakamani na mahakama kuamua mali zigawanywe nusu kwa nusu na mumewe asimamie matunzo ya watoto watatu, kitendo ambacho mumewe hakukubaliana nacho.

Inadaiwa kuwa mpaka sasa mume wake ameuza baadhi ya mali zisizo hamishika huku nyumba waliyoijenga pamoja ikiwa imefungwa, na mumewe hajulikani wapi alipo.