Ndoa yavunjwa baada ya mke kunyimwa tendo la ndoa kwa miaka saba

0
61

Mahakama ya Mwanzo mkoani Mbeya imevunja ndoa baina ya Upendo Charlse (40) pamoja na Nashon Sospeter (54) wakazi wa jijini hapo baada ya mke kudai kutopatiwa unyumba na mume wake kwa miaka saba.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Asha Njovu amesema baada ya kusikiliza kwa kina pande zote mbili mahakama iligundua kuwa ndoa hiyo kamwe haiwezi kurekebishwa tena.

“Ndoa inaunganishwa na watu wawili yaani mke na mume, kadhalika ndoa hiyo hiyo inavunjwa na watu hao hao yaani mke na mume,” amesema Njovu

Serikali kuchunguza shisha kuchanganywa na dawa za kulevya

Aidha, mbali na kunyimwa unyumba kwa miaka saba mlalamikaji ambaye ni mke amedai mume wake amemtelekeza pamoja na watoto wake bila kupatiwa huduma zozote za matunzo ikiwemo chakula, malazi na ada kwa ajili ya watoto.

Send this to a friend