Ndugai: Sitagombea Ubunge mwaka 2025

0
43

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema hatagombea tena nafasi ya ubunge katika jimbo la Kongwa jijini Dodoma.

Amesema hayo jana katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshi ya Mtakatifu Michael.

“2025 sitagombea nafasi ya ubunge tena nastaafu, siyo kama nastaafu kwa kushindwa, lakini ni jambo ambalo tayari nilishalipanga kutoka muda mrefu uliopita hivyo tutaendelea kushirikiana kama ambavyo tunashirikiana sasa,” amesema Ndugai.

Ndugai ameongoza jimbo la Kongwa kuanzia mwaka 2000 na kushika nafasi mbalimbali Bungeni ikiwemo Naibu spika wa Bunge na kisha kuachaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 hadi alipojiuzulu nafasi hiyo Januari 6, Mwaka huu.

Send this to a friend