Ndugu washitakiwa kwa mauaji ya msanii AKA

0
67

Ndugu wawili, Siyabonga na Malusi Ndimande wameshtakiwa kwa mauaji ya rapa maarufu wa Afrika Kusini, Kiernan Forbes (AKA) baada ya kurejeshwa kutoka nchi Eswatini, ambapo wataungana na washitakiwa wengine watano.

Pia wanakabiliwa na mashtaka mengine ya mauaji ya mpishi Tebello “Tibz” Motsoane, ambaye ni rafiki wa karibu na AKA, kujaribu kuua, na kumiliki bunduki kinyume cha sheria.

Ndugu hao waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Durban siku ya Jumanne chini ya ulinzi mkali wa polisi, huku mikono na miguu yao vikiwa vimefungwa pingu.

AKA aliuawa nje ya mgahawa katika jiji la pwani la Durban mwaka 2023. Wakati wa mauaji yake, alikuwa Durban kutumbuiza wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.

Send this to a friend