NEC: Wanasiasa watakaoshindwa kuthibitisha madai ya vituo hewa kuchukuliwa hatua

0
13

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema itawachukulia hatua stahiki wanasiasa na wagombea wanaodai kuwepo kwa vituo na wapigakura hewa endapo watashindwa kuthibitisha madai hayo.

Akizungumza na waandishi wa bahari Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Wilson Charles amesema tuhuma hizo zinalenga kuzua taharuki kwa jambo ambalo si la kweli.

Akieleza sababu ya vituo vya kupigia kura kuwa vingi kuliko vile vya kujiandikisha kupiga kura, Dkt. Mahera amesema hilo limetokana na kila kituo kuwa na idadi ya wapigakura wasizidi 500 ili kurahisisha zoezi la upigaji kura.

“Vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura vilikuwa 37,814, na vituo vya kupigia kura ni 80,155, hii inatokana na kwamba kwenye kituo kimoja kilichotumika kujiandikisha kinaweza kutoa vituo vitatu kwa sababu kituo kimoja kinatakiwa kuwa na wapigakura 450 hadi 500.”

Akizungumzi maandalizi ya upigaji kura amesema tayari vifaa vyote muhimu vimefika kwenye majimbo ya Tanzania Bara na Zanzibar, na kwamba zoezi hilo litafanyika kwa ufanisi.

Send this to a friend