NEC yakanusha uwepo wa kura feki Kawe

0
37

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa madai yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusj kukamatwa kwa kura feki si katika majimbo ya Kawe mkoani Dar es Salaam, Pangani mkoani Tanga na Buhigwe mkoani Kigoma.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa zoezi la kupiga kura.

“Taarifa za madai hayo ya jumla na ambayo siyo rasmi, hayajathibitishwa na hayaelezi ni vituo gani vinahusika na matukio hayo.”

Tume imewataka Watanzania kupuuza taarifa hizo ambazo hazijawasilishwa kwa mamlaka hiyo yenye dhamana ya kusimamia uchaguzi wa wabunge, madiwani, wawakilishi na Rais wa Tanzania.

Send this to a friend