NEC yakubali rufaa za wagombea Ubunge 15

0
41

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewarejesha katika orodha ya wagombea Ubunge wagombea 15 baada ya kupitia nyaraka na kukubali rufaa walizowasilisha.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Charles Mahera ambapo amesema kuwa wametoa uamuzi wa rufaa 55 za wagombea ubunge.

Aidha, NEC imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa na pia imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.

Mahera amesema kuwa tume imechambua vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa vilivyowasilishwa ili kuhakikisha inatenda haki wa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Tume imeongeza kuwa itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo.

Send this to a friend