NECTA: Uchunguzi ufanywe wanafunzi kufeli mitihani
Kaimu Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani ya Taifa (NECTA), Athumani Amasi ameshauri uchunguzi ufanyike ili kujua kwanini ufaulu wa kidato cha pili na darasa la saba umeshuka.
Pia, ameshauri uchunguzi ufanyike kubaini kwanini miaka ya hivi karibuni kumekuwa na udanganyifu kwenye mitihani kiasi cha watu kubadilisha namba za watahiniwa pamoja na kuandika matusi kwenye mitihani.
“Naweza kuoneka wa ajabu kidogo kwa sababu ya utamaduni wetu. Huwa si watu wa kufanya uchunguzi, lakini hii kwa wenzetu wangelifanya haraka sana halafu wangekuja na majibu,” amesema.
CHADEMA yatangaza tarehe ya kuanza kwa mikutano ya hadhara
Aidha, amependekeza kuwa “Tanzania ina wasomi wengi ambao wamekaa tu, huu sasa ni wakati wa kuwaingiza kwenye mtihani wa kufanya uchunguzi.”
Amasi ameeleza kuwa wanaweza kukaa na wanafunzi hao kirafiki na kuwauliza ni nani anawapa mitihani, vivyo hivyo kwa wale wanaotukana wanafanya hivyo kwa sababu gani na kipi huwa kinawasibu.