NECTA yatoa ratiba ya mitihani ya kidato cha sita, diploma na ualimu

0
82

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza ratiba ya mitihani ya ngazi za kidato cha sita, vyuo vya ualimu na stashahada.

Mitihani hiyo itaanza Juni 29 mwaka huu, ikiwa ni muda wa wiki nne tangu taasisi hizo zitakapoanza masomo, Juni 1.

Hatua hii inafuatia uamuzi wa serikali kufungua vyuo vyote nchini, na kuwaruhusu wanafunzi wa kidato cha nne kurejea shule kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya kuhitimu elimu ya sekondari.

Send this to a friend