Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesema gari linaloonekana katika video inayosambaa katika mitandao ya kijamii si lao.
Baraza limeeleza kuwa hujitangaza kwa njia mbalimbali ikiwemo kuandaa na kusambaza kava za matairi (wheel covers) zenye ujumbe wa mazingira kwa wadau wake kama linaloonekana kwenye gari hilo, ila sio gari lao.
Serikali yasitisha mikopo ya 10% katika halmshauri
“Kwa mantiki hiyo kuonekana kwa gari hilo lenye kava ya tairi yenye nembo ya NEMC, haimaanishi kuwa gari hilo linamilikiwa na baraza. Hivyo, NEMC inapenda kuwasihi wananchi kupuuzia video hiyo iliyoleta taharuki na kuchafua taasisi ya Serikali,” imeeleza taarifa.
Aidha, imesema magari yote ya NEMC yana namba za usajili na kufanyiwa matengenezo katika gereji iliyoingia mkataba wa kisheria wa kutoa huduma husika.