NEMC kuzishughulikia kumbi za starehe zinazopiga kelele usiku

0
35

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa onyo kali kwa baadhi ya wamiliki wa kumbi za starehe wanaondelea kukaidi sheria na maelekezo ya baraza hilo juu ya kelele zinazopitiliza kiwango kwenye makazi ya watu nyakati za usiku.

Mkurugenzi wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema kuwa, licha elimu kuendelea kutolewa kwa umma juu ya kelele na athari zinazojitokeza kwenye mazingira, baadhi ya wamiliki wa kumbi za starehe na nyumba za ibada bado wameendelea kukaidi sheria zilizowekwa.

“Sisi kama baraza tunaendelea kusimamia sheria za hifadhi na usimamizi wa mazingira ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa utulivu na amani kwenye maeneo yao na hatutasita kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaoshindwa kufuata taratibu zilizowekwa,”amesema Gwamaka.

Aidha, Dkt. Gwamaka amesema mpaka sasa vyombo vya wamiliki wa kumbi tatu za starehe katika Wilaya ya Temeke na Kinondoni vimekamatwa kwa kushindwa kufuata sheria.

Send this to a friend