New Zealand: Waziri wa Sheria ajiuzulu baada ya kuendesha gari akiwa amelewa

0
46

Waziri wa Sheria kutoka nchini New Zealand, Kiri Allan amejiuzulu mara moja baada ya kukabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari akiwa amelewa na kusababisha ajali pamoja na kukataa kuandamana na polisi mara alipokamatwa.

Baada ya kukamatwa, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 39, alizuiliwa kituoni kwa saa nne kabla ya kuachiliwa, na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni kwa madai hayo.

Hakuna majeruhi walioripotiwa kutokana na ajali hiyo, ambayo ilitokea jijini Wellington usiku wa Jumapili.

Kulingana na Newshub, Bi Allan alisema katika taarifa yake kwamba amekuwa akipitia matatizo binafsi katika wiki za hivi karibuni yaliyopelekea kutokuwa katika hali yake ya kawaida, ambapo mwezi uliopita aliuthibitishia umma kuhusu kutengana na mwenzi wake na pia anakabiliwa na tuhuma za kushindwa kuwa na uhusiano mzuri na wafanyakazi wake.

Raila Odinga asitisha maandamano ya Jumatano

“Nilichukua muda wa mapumziko ili kushughulikia mambo hayo na niliamini nilikuwa sawa kushughulikia changamoto hizo pamoja na shinikizo la kuwa Waziri. Matendo yangu jana [Jumapili] yanaonesha kuwa sikuwa sawa na nimewaangusha mimi na wenzangu,” amesema.

Yeye ni waziri wa nne kutoka baraza la mawaziri la Waziri Mkuu, Chris Hipkins kujiuzulu tangu mwezi Machi kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Allan alikuwa akionekana kama kiongozi mpendwa ndani ya chama cha Labour na hata alitabiriwa kumrithi aliyekuwa waziri mkuu wa zamani, Jacinda Arden ambaye alijiuzulu mwaka huu kabla ya Hipkins kuchukua nafasi yake.

Send this to a friend