Ney wa Mitego ashitakiwa kwa uchochezi

0
48

Msanii Emmanuel Elibariki maarufu ‘Nay wa Mitego’ ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi kupitia wimbo wake wa ‘Amkeni’.

Akiambatana na wakili wake Jebra Kambone, Ney wa Mitego amesema ameachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano yaliyochukua takribani saa tatu na kukamilisha masharti aliyopewa.

Ney wa Mitego alifika katika Kituo cha Polisi Central, Dar es Salaam baada ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano.

Hata hivyo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema halihusiki na kuitwa kwake polisi licha ya kwamba wamemuita mara kadhaa kufika katika ofisi hizo lakini hakuitikia wito huo.

“Tumetoa wito mara mbili kwa ajili ya maadili ya kawaida tu lakini kwa bahati mbaya sana hakuwahi kutokea, na jana tumeandika wito mwingine tukimtaka aje Ijumaa saa 4 asubuhi hajatujibu, sijui kama atakuja ama hatokuja.

Mambo ya polisi nafikiri hayo ni masuala ya kijinai, sisi tunahusiana na masuala ya Sanaa tu wala hatuna jukumu la kwenda kumshitaki,” amesema Mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamugisha.

Send this to a friend