Ng’ombe 70 zakamatwa zikisafirishwa nje ya nchi kinyume na sheria

0
31

Jeshi la Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo mkoani Arusha kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi limewakamata watuhumiwa wanne na ng’ombe 70 ambao walikuwa wakitoroshwa kwenda nchi jirani kinyume na utaratibu.

Akitoa taarifa hiyo wilayani Longido mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Simon Pasua amesema watuhumiwa hao waliokamatwa majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi huku akiweka wazi kuwa kikosi hicho tayari kina majina ya watu wanajihusisha na utoroshaji wa mifugo ambao pia watakamatwa wakati wowote.

Aidha, Kamanda Pasua amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu wanaojihusisha na utoroshaji wa mifugo ili jeshi hilo liwachukulie hatua za kisheria wahusika wa vitendo hivyo.

Send this to a friend