NGOs 4,900 hatarini kufutwa na serikali

0
25

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju ameyataka zaidi ya mashirika 4,900 yaliyokiuka sheria na taratibu zinazoyaongoza yeleze sababu kwanini yasifutiwe usajili ndani ya mwezi mmoja.

Ameyasema hayo mkoani Iringa katika ziara yake ya siku mbili yenye lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya wizara.

Mpanju amesema mashirika hayo yameshindwa kutekeleza matakwa ya kisheria ikiwemo kuwasilisha taarifa zao kwa ajili ya uhakiki, na kueleza kuwa tangu uhakiki huo uanze mwaka jana, mashirika hayo hayakufanya hivyo.

“Hadi kazi hiyo inakamilika Machi mwaka huu, ni mashirika 4,864 kati ya 12,884 yamehakikiwa, na mashirika 7,533 ndiyo yako hai. Niwaombe NaCONGO (Baraza na Mashirika yasiyo ya kiserikali) hakikisheni yale mashirika ambayo hayakuhakikiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, yaeleze kwanini yasifutiwe ndani ya mwezi mmoja. Hapa Iringa ni ,mashirika 79 kati ya 170,” alisema Mpanju.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali inafanya uhakiki ili kuhakikisha uratibu wa mashirika unakuwa na ufanisi, na pia ni matakwa ya sheria ya nchi.

Send this to a friend