NHIF yarejesha dawa 178 zilizoondolewa

0
43

Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF), umerejesha dawa 178 pamoja na kujumuisha dawa nne zilizokuwepo kwenye mwongozo wa Taifa wa matibabu lakini hazikuwemo kwenye Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (NEMLIST) ambapo umezijumuisha dawa hizo kwenye Kitita chake cha Mafao cha Mwaka 2023.

Katika taarifa ya NHIF iliyotolewa kwa umma, imeeleza kuwa hatua hiyo inaongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwa wanachama kwa kuzingatia miongozo ya tiba nchini.

“Kutokana na maboresho hayo, Mfuko wa Taifa Bima ya Afya unawahakikishia wanachama wake kuwa huduma za matibabu zitaendelea kupatikana katika vituo vyote vilivyosajiliwa nchi nzima. Endapo kutakuwa na changamoto za kiutekelezaji mfuko unashauri vituo vya kutoa huduma viwasiliane na ofisi za mfuko kuepuka usumbufu usio wa lazima kwa wateja wao,” imeeleza taarifa.

Serikali yapiga marufuku uvutaji sigara maeneo ya wazi

NHIF imeongeza kuwa iwapo mwanachama atakutana na changamoto yoyote katika upatikanaji wa huduma anashauriwa kuwasiliana na mfuko kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu bila malipo namba 199.

Send this to a friend