NHIF yasitisha mabadiliko katika utoaji huduma

0
44

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesitisha utekelezaji wa mabadiliko mbalimbali katika mfumo wake wa utoaji huduma kuanzia Agosti 03, 2022 mpaka hapo itakapotoa taarifa.

Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Celestin Muganga, maboresho hayo yalikuwa na lengo la kuepusha matumizi ya huduma za bima ya afya yasiyo sahihi, na hivyo kuongeza gharama zisizo za lazima.

Muganga amesema katika hatua za awali za utekelezaji, kumejitokeza changamoto ambazo zimesababisha usumbufu usiotarajiwa kwa wadau wa mfuko huo.

Hivyo, kutokana na hali hiyo mfuko umepokea maoni na ushauri juu ya namna bora ya kutekeleza maboresho hayo na kuanza kuyafanyia kazi bila kuathiri upatikanaji wa huduma kwa wanufaika wake.

Send this to a friend