NHIF yatoa sababu ya kuondoa kifurushi cha Toto Afya Kadi

0
36

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), imesema watoto ambao awali walikuwa wakisajiliwa kupitia utaratibu wa bima ya afya ya ‘Toto Afya Kadi,’ sasa watasajiliwa kupitia vifurushi vya bima ya afya au shule wanazosoma ili kufanya maboresho zaidi ikiwemo malalamiko yanatolewa na wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga amesema wakati wa maboresho hayo watoto waliolipia kadi zao wataendelea kupata matibabu lakini kwa wale ambao wanataka kujiandikisha watasajiliwa kupitia shule zao.

“Tunashukuru mpaka sasa tuna shule nyingi tu ambazo zimeonesha nia na wengine kwao ni fursa kuvutia watoto shuleni wameshaanza kuja maofini kwetu na kutafuta namna bora ya kushirikiana na hizo shule ili sasa waweze kuingiza watoto kwa umoja wao,” amesema

Watu 4,060 wamefariki kwa ajali za barabarani nchini tangu mwaka 2020

Konga amesema faida moja wapo ya kusajili mashuleni ni dhana ya bima ya afya kujengeka mapema kwa watoto, matarajio ya kusajili watoto wengi yatafikiwa lakini pia wakati maboresho yanafanywa kwenye eneo la usajili na huduma Watoto wanaotaka kuingia hawatoweza kukosa huduma zinazotarajiwa.

“Tunafahamu mafaniko ni makubwa, sasa hivi watoto wote kuanzia shule ya msingi mpaka form six wako shuleni wanasoma. Mtoto atasajiliwa kupitia shule, atasajiliwa kupitia mzazi wake. Lakini pia tunafahamu kama wale masikini ambao wako kwenye makazi basi nao tutawafuata kupitia makazi,” amefafanua.

Aidha, amewataka wazazi kushirikiana na NHIF kwa kutoa taarifa ikiwa watapata ugumu wowote katika kusajiliwa kwa watoto wao shuleni.

Send this to a friend