NI BALAA! VODACOM YAJA NA HUDUMA ZA MATENGENEZO YA SIMU KWA WATEJA WAKE

0
49

Vodacom Tanzania imekuja na huduma mpya kwa wateja wake kwa kuzindua vituo vya huduma za matengenezo ya simu kwa ushirikiano na watengenezaji wa simu za Neon Ultra, Samsung, Vivo, Motorola, Honor na Oppo.

Lengo ni kusogeza huduma bora kwa wateja ikiwemo kupata matengenezo ya simu zao katika maduka ya Vodacom katika maeneo mbalimbali nchini huku duka la Vodacom Mlimani City likiwa kama mfano wa huduma hizo ambazo ni za kwanza nchini kutoka kwa kampuni ya mawasiliano.

Send this to a friend