Niger yakata uhusiano wa kidiplomasia na Nigeria, Ufaransa, Marekani na Togo

0
13

Serikali ya kijeshi nchini Niger imetangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi nne ambazo ni Nigeria, Togo, Marekani na Ufaransa kutokana na mazungumzo na ECOWAS yaliyolenga kutafuta suluhisho kutozaa matunda.

Katika hotuba ya runinga ya serikali ya Niger (RTN), Kanali Amadou Abdraman amesema kazi za mabalozi na wawakilishi wa Jamhuri ya Niger nchini Ufaransa, Nigeria, Togo, na Marekani zimesitishwa.

“Kazi za mabalozi wa Jamhuri ya Niger nchini Ufaransa, Nigeria, Togo na Marekani zimesitishwa. Misimamo yote ya awali ambayo ni tofauti na amri hii inafutwa,” amesema Kanali Abdramane.

Ujumbe wa majadiliano uliongozwa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu wa Nigeria, Jenerali Abdulsalami Abubakar ambaye alikutana na baadhi ya viongozi wa mapinduzi, lakini aliondoka saa chache baadaye akionesha kutokuwa na mafanikio.

Viongozi wa kijeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanatarajiwa kuhitimisha kikao cha siku tatu nchini Nigeria ambacho kinaangalia uwezekano wa kuvamia kijeshi endapo diplomasia itafeli.

Send this to a friend