Niger yamfukuza Balozi wa Ufaransa

0
36

Kikosi cha jeshi cha Niger kimeamuru Balozi wa Ufaransa kuondoka nchini humo ndani ya saa 48 baada ya kushindwa kuhudhuria mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika Ijumaa huko Niamey na Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger.

Kupitia taarifa iliyochapishwa na kituo cha televisheni kinachosimamiwa na serikali, ORTN, Wizara ya Mambo ya Nje ya Niger imeeleza kuwa mamlaka ya Niger iliamua kuondoa utambulisho wa Balozi Sylvain Itte kutokana na kukataa kwake kuhudhuria mkutano huo.

Aidha, wizara imesema sababu nyingine iliyopelekea kuchukuliwa kwa hatua hiyo ni kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Ufaransa zilizopingana na maslahi ya Niger.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imejibu kwa kusema kwamba “Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesikia ombi la waasi. Waasi hawana mamlaka ya kutoa madai haya, idhini ya balozi inatoka kwa mamlaka halali na walioteuliwa kihalali nchini Niger.”

Send this to a friend