Nigeria: Azam yazuiwa kurusha mechi ya Rivers United na Yanga

0
51

Azam Media imesema kwamba haitorusha mbashara matangazo ya moja kwa moja ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Rivers United na Yanga SC utakaopigwa leo nchini Nigeria.

“Tunasikitika kuwaarifu kwamba, hatutaweza kuwaletea matangazo ya moja kwa moja ya mchezo wa CAF Champions League kati ya Rivers United na Yanga SC,” wameeleza kupitia ukurasa wao wa Twitter.

Azam wamesema wamejitahidi kwa kila namna kuweza kununua haki za matangazo hayo toka kwa Rivers United, lakini imeshindikana kwa sababu Rivers United hawataonesha mchezo huo mbashara.

Licha ya kukataliwa pia kurusha matangazo kwa njia ya sauti, wamesema kupitia watumishi wake waliopo Nigeria watatoa taarifa za mechi hiyo wakati wa matangazo ya Simba Day.

Send this to a friend