Nigeria: Mama wa Osinachi Nwachukwu aeleza vitisho alivyopokea toka kwa mkwewe

0
56

Kwa mara ya kwanza mama wa aliyekuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Nigeria, Osinachi Nwachukwu, Bi. Madu amezungumza kuhusu kifo cha mwanae na kusema kuwa binti yake aliondoka kwa mume wake baada ya mateso aliyokuwa akipitia, lakini mumewe na mchungaji walimsihi arudi.

Akizungumza na Shirika la habari BBC, Bi. Madu ameonesha kusikitishwa na mkwewe wake Peter Nwachukwu na kueleza kuwa, binafsi hakutaka mwanae arudi kwa mume wake maana tangu alipoolewa na mume huyo, hawakuwa na amani, hivyo alitaka aendelee kukaa nyumbani na atafute mume wa kumuoa.

“Ninaumia kwa ajili ya huyu mkwe wangu, alikuja hapa kwa ajili ya kutaka kumuoa mwanangu na nikampatia ushirikiano, lakini sasa amechukua uhai wake,” amesema.

Bi Madu ameeleza kuwa siku moja mume wa Osinach aliwapigia simu na kuwaeleza kuwa, ikiwa mtoto wao hatorudi akiwa hai basi atarudi akiwa amekufa.

Maneno hayo yalimfanya dada yake mkubwa Favour Mmadu kusafiri hadi Abuja kumchukua Osinach ili kurejea nae nyumbani na ndipo alikaa kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu kabla ya mumewe  na mchungaji kumuomba arejee tena kwenye ndoa yake.

Send this to a friend