Nigeria: Mume wa mwimbaji Osinach Nwachukwu ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

0
50

Aliyekuwa mume na meneja wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Nigeria, Peter Nwachukwu amehukumiwa kunyongwa mpaka kufa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Osinach Nwachukwu, kinyume na kifungu cha 221 cha kanuni ya adhabu.

Inadaiwa kifo cha mwimbaji huyo kilitokana na kipigo kutoka kwa mumewe na kupelekea kulazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Baada ya taarifa ya awali iliyoripoti kuwa kifo chake kilitokana na kansa ya koo, familia ilipinga taarifa hizo, na ndipo hospitali ya Taifa ikafanya uchunguzi wa mwili na kukabidhi ripoti kwa polisi.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Sinachi zinasema, marehemu alikuwa na uvimbe wa damu ulioganda kwenye kifua uliopelekea kifo chake.

Akiwa mahakamani, imeelezwa kwamba Nwachukwu alimnyima marehemu uhuru wa kibinafsi na kumzuia kutembea, matusi, kumwathiri kisaikolojia, pia alimnyima pesa za kujitibia baada ya kumpiga na kumlazimu kuomba na kukopa kwa watu.

Hata hivyo, licha ya kuwa meneja wake katika muziki inadaiwa hakumruhusu kwenda katika matamasha ya kuimba ilimradi asionekane licha ya kuwa alikuwa amelipwa tayari, hiyo ilipelekea waandaji wa maonesho kutokumualika kwa ajili ya huduma ya uimbaji.

Send this to a friend