Nigeria: Mume wa mwimbaji Osinachi akamatwa na Polisi

0
40

Mume wa aliyekuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Nigeria, Marehemu Osinachi Nwachukwu amekamatwa kufuatia kifo cha mkewe kinachodaiwa kuwa kinatokana na kuwa mwathirika wa unyanyasaji.

Msemaji wa polisi jijini Abuja amenukuliwa na tovuti za Daily Trust and Punch akithibitisha kukamatwa kwa Peter Nwachukwu baada ya malalamiko kutoka kwa kaka wa mwimbaji huyo.

Taarifa zinasema, Osinachi (42) ambaye alipoteza maisha siku ya Ijumaa akiwa hospitalini katika mji mkuu wa Abuja, aliripotiwa awali kuwa alikuwa akiugua saratani ya koo, lakini familia yake imekanusha hilo.

Osinachi alikuwa mwimbaji mkuu wa Dunamis International Gospel Centre, alipata umaarufu kupitia wimbo wa injili wa Ekwueme alioshirikiana na Prospa Ochimana mwaka 2017.

Send this to a friend