Nigeria: Rais amteua marehemu kushika wadhifa serikalini

0
39

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amemteua mtu aliyefariki kushika wadhifa serikali, jambo ambalo limeibua mjadala nchini humo huku baadhi wakidai ofisi hiyo haipo makini.

Jina la Tobias Chukwuemeka aliyefariki miezi miwili iliyopita lilikuwa miongoni mwa majina 37 ya waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bodi ya wakala wa serikali yaliyowasilishwa kwenye seneti ya nchi hiyo kwa ajili ya kuhakikiwa.

Msaidizi wa rais, Laurretta Onochie amesema kuwa wakati uteuzi huo unafanyika Februari mwaka huu, Chukwuemeka alikuwa hai, na pia aliwasilisha wasifu wake kwa ajili ya kutangazwa mara seneti itakaporidhia majina hayo.

“Alipofariki wakati akisubiri uteuzi huo, serikali kuu haikupewa taarifa za kifo chake,” amesema Onoiche.

Hata hivyo si mara ya kwanza kwa Rais Buhari kufanya kosa kwa kuteua mtu aliyefariki kushika wadhifa fulani. Mwaka 2017 alifanya uteuzi wa wajumbe wa bodi za serikali, ambapo zaidi ya watu wanne walioteuliwa walikuwa wamefariki.

Send this to a friend