Nigeria: Sheikh ahukumiwa kunyongwa kwa kumkufuru Mtume Muhammad

0
58

Mhubiri mashuhuri wa Kiislamu, Sheikh Abduljabar Nasir Kabara amehukumiwa kunyongwa hadi kufa na mahakama katika jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria baada ya kumkuta na hatia ya kumkufuru mtume Muhammad pamoja na uchochezi katika baadhi ya mahubiri yake.

Sheikh Kabara anashikiliwa na mamlaka tangu Julai mwaka jana baada ya kutuhumiwa kueneza mahubiri ya uongo dhidi ya Mtume.

Kesi hiyo inafuatiliwa kwa karibu na Wanigeria akiwa na idadi kubwa ya wafuasi hasa katika jimbo la Kano ambapo baba yake alikuwa kiongozi wa dhehebu hilo huko Afrika Magharibi hadi kifo chake mnamo 1996.

Mchungaji afariki baada ya kufunga kwa siku 8 bila kula

Aidha, Sheikh Kabara mwenye umri wa miaka 52 anayetokea katika madhehebu ya Qadiriyya ana haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Hukumu za kifo nchini Nigeria hutekelezwa kwa nadra, hivyo watu waliohukumiwa kifo huwekwa magerezani kwa muda usiojulikana.

Send this to a friend