Nigeria yapiga marufuku magari yenye vioo ‘tinted’

0
74

Katika jimbo la Kusini-Mashariki la Enugu nchini Nigeria, mamlaka zimepiga marufuku matumizi ya magari yenye vioo vilivyokuwa ‘tinted’ ikiwa ni jitihada za kupunguza uhalifu nchini humo.

Kwa mujibu wa afisa wa Serikali ya jimbo, wamiliki wa magari yenye vioo vya hivyo, wamepewa muda hadi Septemba 4 mwaka huu ili kupata kibali kutoka kwa polisi na baada ya hapo mamlaka hazitasita kuwakamata na kuwatoza faini.

Matumizi ya magari yenye vioo ‘tinted’ ni maarufu huko Enugu kwani pia hutumiwa na wahalifu kufanya uhalifu kama vile wizi na utekaji nyara.

Taarifa hiyo imepokelewa vyema na baadhi ya wafanyabiashara wa magari katika jimbo hilo wakieleza kuwa wahalifu wanafunika madirisha ya magari yao kutoka kwa wauzaji wasio rasmi hivyo kufanya uhalifu kwa urahisi

“Ikiwa unataka gari lako liwe na madirisha tinted unahitaji kibali, unapeleka gari lako kwa polisi. Ikiwa dirisha tinted ni la kiwandani, watakupa leseni na watakuwa na data yako ili ikitokea chochote, wanaweza kukuita kwa mahojiano,” amesema Collins P, mmiliki wa kampuni ya magari.