Nissan kuuza magari ya umeme pekee ifikapo mwaka 2030

0
68

Kampuni ya magari ya Japan, Nissan, imeahidi kuendelea na mpango wake wa kuuza magari ya umeme pekee barani Ulaya ifikapo mwaka 2030 hatua iliyotajwa kuwa muhimu katika kupambana na uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Hii inamaanisha kuwa wateja wa Nissan barani Ulaya watarajie kuona mifano mpya ya magari ya umeme katika soko badala ya magari yanayotumia injini za petroli au dizeli.

Hata hivyo, tangazo hilo linakuja baada ya hatua ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak kusogeza mbele katazo la mauzo mapya ya magari yanayotumia petroli na dizeli kwa muda wa miaka mitano kutoka 2030 hadi 2035.

ATCL: Boeng 787-7 (Dreamliner) mbili ziko kwenye matengenezo

Kampuni za magari tayari zimeshatumia mabilioni ya fedha kufanya mabadiliko katika mifano ya magari wanayotengeneza na katika njia wanazosambaza magari hayo ili kuwa na magari ya umeme badala ya kutumia petroli au dizeli.

Nissan ina mpango wa kupeleka sokoni mifano 19 ya magari yanayotumia umeme na nane za haidrojeni kabla ya kufikia mwaka 2030, na kufikia mwaka 2028 inakusudia kuwa na teknolojia isiyokuwa na kobalti ambayo itapunguza gharama za betri za magari ya umeme kwa asilimia 65.