Njia 3 rahisi za kuondoa harufu mbaya kwenye gari lako

0
37

Harufu mbaya ndani ya gari huweza kusababishwa na sababu za kiufundi ikiwemo hitilafu za umeme au matatizo kwenye injini. Iwapo matatizo hayo hayatopewa ufumbuzi yanaweza kuleta athari kiafya.

Wataalam wa magari wanasema kupulizia manukato kwenye gari lako hakutatui tatizo bali hupunguza kwa muda mfupi au pengine kuongeza tatizo zaidi.

Hizi ni njia tatu za kuondoa harufu kwenye gari lako;

Baking soda
Ili kuondoa harufu kwenye gari lako unachotakiwa kufanya ni kuwa na chupa ya baking soda na kisha utoboe matundu kadhaa kwa juu na uiacha kwenye gari na uifanye kama kiondoa harufu cha asili.

Siki
Mimina siki kwenye kikombe na ukiache kikombe kwenye gari lako usiku mzima. Kwa kufanya hivyo itaondoa harufu yote na pia unaweza kuitumia kufuta sehemu yenye harufu kwa kutumia siki iliyochanganywa na maji.

Mkaa
Mkaa ni dawa ya asili ambayo itakusaidia kufyonza hewa mbaya katika gari lako. Unachotakiwa kufanya ni kuuweka katika mfuko na kuuacha wazi usiku kucha kisha utaona maajabu.

Send this to a friend