Njia 3 rahisi za kuondoa hofu katika siku yako ya harusi

0
64

Je! Unahisi wasiwasi na woga juu ya siku yako ya harusi? Inaeleweka kwa kuwa hiyo ni siku kubwa kwako na kwa mtarajiwa wako. Unaweza pia kuwa na wasiwasi ukihofia kwamba utakuwa ukitazamwa na watu wote siku hiyo. Ikiwa unapata hofu kuhusu kukutana na watu au kuzungumza hadharani, zingatia ushauri huu ili kufurahia siku yako ya harusi.

Kumbuka ni harusi, sio maonesho
Wachumba wengi (na maharusi pia) wamekuwa wakichukulia na kuona siku ya harusi yao kama onesho. Njia hii ya kufikiria inaweza kukupa wasiwasi zaidi na hofu kwenye siku yako kuu.

Wageni ambao watahudhuria harusi yako wanatarajia jambo moja tu, kukuona wewe na bibi harusi wako mkiapa viapo vyenu na kuoneshana upendo. Kwa hivyo usijali ikiwa utafanya makosa kwa kuwa kila mtu katika siku yako atakuwa upande wako.

Iwapo utakosea au kuchanganyikiwa kuhusu kile unachopaswa kufanya, watakuwa nyuma yako kukuunga mkono. Hawa ni wapendwa wako, familia yako na marafiki zako.

Linapokuja suala hilo, watakachojali zaidi ni kumbukumbu za furaha. Wataenda nyumbani wakizungumza jinsi chakula kilivyokuwa kizuri, jinsi nyinyi wawili mlivyopendeza, na sio wakati mfupi ambapo ulionekana kukosea.

Fanya mazoezi, fanya mazoezi, fanya mazoezi
Unaweza kuwa unaogopa kuongea hadharani lakini ukweli ni kwamba unaweza kuondokana na hofu hiyo kwa mazoezi pekee. Kadiri unavyokariri jambo hilo (mfano hotuba), ndivyo unavyojiamini zaidi na ndivyo utakavyoanza kustarehe kuhusu harusi yako.

Omba ushauri
Omba ushauri kwa mtu ambaye hahusiki moja kwa moja kwenye harusi, ujuzi na uelewa wake unaweza kukusaidia kutuliza hofu yako na kukusaidia kufurahia siku yako kuu.

Send this to a friend