Katikati ya ukungu wa vita, inaweza kuwa ngumu kuona njia ya kusonga mbele. Kwa Mujibu wa Mwandishi wa Habari za Kidemokrasia, Mwingereza James Landale anaeleza baadhi ya njia ambazo zinaweza kuwa ndio mwisho wa vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine.
1. Vita fupi
Urusi iimarishe operesheni zake za kijeshi kwa mashambulizi makubwa zaidi. Maelfu wafe, Kyiv inaanguka, Rais wa Ukraine anauawa au anatoroka, na Urusi inaweka serikali ya vibaraka inayounga mkono Moscow.
Haya yatakuwa matokeo yasiyo thabiti, ambayo yanaweza kuathiriwa na uasi na migogoro ya siku zijazo.
2. Vita vya muda mrefu
Baada ya kutwaa maeneo, morali ya jeshi la Urusi inashuka kutokana na kukosa mahitaji ya msingi. Hii inaweka mazingira ya kutawala maeneo waliyoyatwaa kuwa mgumu. Baada ya muda wapiganaji wa Ukraine wanaanzisha mashambulizi, huku nchi za Magharibi zikiendelea kuwapatia silana
Pengine baada ya miaka mingi mbeleni Urusi inaamua kuondoka.
3. Vita vya Ulaya
Putin anaweza kutuma wanajeshi katika jamhuri za zamani za Sovieti kama Moldova na Georgia, ambazo si sehemu ya NATO. Putin anaweza kuchukua njia hiyo ya hatari akiona ndio namna pekee anaweza kuunusuru uongozi wake endapo ataona anashindwa vita. Kwa kupeleka majeshi kwenye nchi hizo inaweza ikazua hatari zaidi na vita ikahusisha nchi nyingi za Ulaya.
4. Suluhisho la kidiplomasia
Kwa kuwa tayari kukubaliana na mazungumzo – hata kama hayajawa na mafanikio makubwa, lakini Putin anaonesha uwezekano wa kukubali kufanyika mazungumzo kusitisha mapigano. Putin akiona anashindwa, ataona kuwa hiyo ni fedheha kubwa kwake kuliko fedheha ya kuimaliza kwa njia ya mazungumzo.
5. Putin apinduliwe
Inaweza kuonekana kuwa isiyofikirika. Hata hivyo dunia imebadilika katika siku za hivi karibuni. Ikiwa vita ni mbaya kwa Urusi, kunaweza kuwa na tishio la mapinduzi maarufu. Na ikiwa wale ambao wamefaidika kutoka kwa Putin hawatafikiria tena kuwa anaweza kutetea masilahi yao, matokeo kama haya yanaweza kuwa yasiyowezekana.