Njia 5 za kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa

0
44

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu milioni moja duniani kote wanaambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku. Magonjwa haya yamekuwa yakienezwa zaidi kupitia kujamiiana.

Hizi ni dalili za magonjwa ya ngono kwa wanaume;

•Maumivu wakati wa kukojoa na tendo la ndoa
•Malengelege na vidonda sehemu za siri
•Kutokwa na uchafu usio wa kawaida kwenye uume
•Kuvimba sehemu za siri ikiambatana na maumivu makali

Dalili za magonjwa ya zinaa kwa Mwanamke.

Kwa kiasi kikubwa dalili huchelewa kujionesha kwa wanawake baada ya kupata maambukizi. Endapo dalili zitajitokeza zitakuwa kama;

•Maumivu wakati wa tendo la ndoa na kukojoa
•Muwasho ukeni
•Kutokwa uchafu usio kawaida ukeni
•Malengelenge na vipele sehemu za siri na mdomoni

Fanya mambo haya ili kujilinda dhidi ya magonjwa hayo;

Jali Kinga: Tumia kondomu wakati wa kujamiana na epuka shughuli zozote za ngono zinazoweza kusababisha jeraha ukeni ambapo hatari ya kuambukizwa ni kubwa.

Subiri ukomavu wa kijinsia kiakili na kihisia: Kadiri mtu anavyokuwa na umri mdogo anapoanza kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza ndivyo inavyokuwa rahisi kwake kupata magonjwa mbalimbali ya zinaa.

Mambo yanayoweza kutokea unapotumia simu wakati unaichaji

Pata Chanjo: Chanjo zinapatikana ili kusaidia kulinda dhidi ya Homa ya Ini (Hepatitis B) na papillomavirus ya binadamu. Chanjo za HPV hutolewa katika umri wa miaka 11-12.

Pombe: Usinywe pombe na kufanya ngono, kwani itakufanya ushindwe kudhibiti tabia za ngono.

Mwone daktari: Usisite kujadili masuala yako na daktari ili kupata ushauri wa namna ya kuepuka magonjwa haya pamoja na tiba upatapo viashiria vya magonjwa ya zinaa.

Send this to a friend