Njia 5 za kujikinga dhidi ya wadukuzi wa mitandao

0
42

Uhalifu wa udukuzi hufanywa kwa nia ya kuiba data. Data hizo zinaweza kuwa taarifa zako za kifedha (ambapo wanaweza kufikia akaunti yako ya benki au mikopo na kutoa pesa), maelezo kuhusu utambulisho wako (ili waweze kuiba utambulisho wako na kufungua akaunti mpya za kifedha chini yako.), au ushahidi wa hatia ambao wanaweza kuwa nao dhidi yako.

Hizi ni Njia 5 za kujikinga na wadukuzi;

Tumia nywila thabiti/imara
Nywila (password) zinapaswa kuwa na mchanganyiko wa herufi, nambari na herufi maalum ili kuzifanya ziwe thabiti iwezekanavyo. Kwa nywila iliyo salama zaidi, unapaswa kuepuka kutumia maneno kama vile majina, maeneo, tarehe, nambari za simu, siku za kuzaliwa, anwani, n.k., kwa kuwa hizi ni rahisi kwa wadukuzi kukisia.

Angalia mara kwa mara matoleo mapya ya programu
Unapofanya mara kwa mara maboresho kwa kuangalia matoleo mapya ya programu (updating) husaidia kuepusha hatari mpya za usalama zinapotokea. Hakikisha unatumia toleo jipya zaidi.

Pakua ulinzi wa antivirus
Programu ya kuzuia virusi husaidia kulinda dhidi ya wadudu ambao wanaweza kujaribu kuambukiza kompyuta yako. Njia bora ya kuhakikisha ulinzi huu ni kupitia michanganuo ya mara kwa mara inayofanywa kiotomatiki na programu ya kingavirusi.

Usifungue Barua pepe ikiwa huna uhakika nazo
Wakati wowote unapopokea barua pepe kutoka kwa mtu usiyemjua, fanya mazoea ya kutowahi kubofya kiungo (link) zilizopachikwa humo. Ikiwa barua pepe inatoka kwa rafiki, mwanafamilia, au biashara unayoifahamu, lakini huna uhakika kama ni halali, wasiliana na mtu huyo kwa barua pepe tofauti au tembelea tovuti ya biashara hiyo moja kwa moja.

Kuwa mwangalifu na ofa za mitandaoni

Usijibu barua pepe zinazotoa ofa za bure au kuuliza taarifa binafsi. Ulaghai huu kwa kawaida huhusisha virusi vilivyoundwa ili kunasa kitambulisho chako cha kuingia.

Send this to a friend